Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 17

Yohana 17:7-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Sasa wanajua kuwa kila kitu ulichonipa mimi kinatoka kwako,
8kwa maneno yale uliyonipatia mimi— Nimekwisha wapatia wao maneno hayo. Waliyapokea na kweli wakajua ya kuwa mimi nimetoka kwako, na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
9Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako.
10Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo.
11Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa sisi ili wao nao wawe na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo na umoja.
12Nilipokuwa nao, niliwalinda kwa jina ulilonipa; Niliwalinda, na hakuna hata mmoja wao aliyepotea isipokuwa mwana wa upotevu, ili kwamba maandiko yatimie.
13Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
14Nimewapa neno lako; ulimwengu imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
15Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
16Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
17Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
18Ulinituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.

Read Yohana 17Yohana 17
Compare Yohana 17:7-18Yohana 17:7-18