Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Yohana 17:7-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Yohana 17:7-18 in Biblia Takatifu

7 Sasa wanajua kwamba kila ulichonipa kimetoka kwako.
8 Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa nao wameupokea; wanajua kwamba kweli nimetoka kwako, na wanaamini kwamba wewe ulinituma.
9 “Nawaombea hao; siuombei ulimwengu, ila nawaombea hao ulionipa, maana ni wako.
10 Yote niliyo nayo ni yako, na yako ni yangu; na utukufu wangu umeonekana ndani yao.
11 Na sasa naja kwako; simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni. Baba Mtakatifu! Kwa nguvu ya jina lako ulilonipa, tafadhali uwaweke salama ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo mmoja.
12 Nilipokuwa nao, mimi niliwaweka salama kwa nguvu ya jina lako ulilonipa. Mimi nimewalinda, wala hakuna hata mmoja wao aliyepotea, isipokuwa yule aliyelazimika kupotea ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia.
13 Basi, sasa naja kwako, na nimesema mambo haya ulimwenguni, ili waweze kushiriki kikamilifu furaha yangu.
14 Mimi nimewapa neno lako, nao ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao si wa ulimwengu kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
15 Siombi uwatoe ulimwenguni, bali naomba uwakinge na yule Mwovu.
16 Wao si wa ulimwengu, kama vile nami nisivyo wa ulimwengu.
17 Waweke wakfu kwa ukweli; neno lako ni ukweli.
18 Kama vile ulivyonituma ulimwenguni, nami pia nimewatuma wao ulimwenguni;
Yohana 17 in Biblia Takatifu

Yohana 17:7-18 in Biblia ya Kiswahili

7 Sasa wanajua kuwa kila kitu ulichonipa mimi kinatoka kwako,
8 kwa maneno yale uliyonipatia mimi— Nimekwisha wapatia wao maneno hayo. Waliyapokea na kweli wakajua ya kuwa mimi nimetoka kwako, na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.
9 Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako.
10 Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo.
11 Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa sisi ili wao nao wawe na umoja, kama vile mimi na wewe tulivyo na umoja.
12 Nilipokuwa nao, niliwalinda kwa jina ulilonipa; Niliwalinda, na hakuna hata mmoja wao aliyepotea isipokuwa mwana wa upotevu, ili kwamba maandiko yatimie.
13 Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.
14 Nimewapa neno lako; ulimwengu imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu
15 Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.
16 Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.
17 Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika Kweli; neno lako ndiyo kweli.
18 Ulinituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.
Yohana 17 in Biblia ya Kiswahili