Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi - Waamuzi 6

Waamuzi 6:1-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wana wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; naye akawatia mikononi mwa Midiani kwa miaka saba.
2Uwezo wa Midiani uliwanyanyasa Israeli. Kwa sababu ya Midiani, watu wa Israeli walitengeneza makao wenyewe kutoka kwenye mabwawa katika milima, mapango, na ngome.
3Kisha ikawa kwamba wakati wowote Waisraeli walipopanda mazao yao, Wamidiani na Waamaleki na watu kutoka mashariki waliwavamia Waisraeli.
4Waliweza kutengenezajeshi lao juu ya ardhi na kuharibu mazao, mpaka njia ya Gaza. Hawakuacha chakula huko Israeli, wala kondoo wala ng'ombe wala punda.
5Kila wakati wao na mifugo yao na mahema walipokuja, walikuja kama kundi la nzige, na haikuwezekana kuhesabu watu au ngamia zao. Walivamia ardhi ili kuiharibu.
6Midiani iliwadhoofisha Waisraeli sana mpaka watu wa Israeli wakamwita Bwana.
7Watu wa Israeli walipomwomba Bwana kwa sababu ya Midiani,
8Bwana alimtuma nabii kwa wana wa Israeli. Nabii akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekuleta kutoka Misri; Nilikutoa nje ya nyumba ya utumwa.
9Naliwaokoa kutoka kwenye mikono ya Wamisri, na kutoka kwenye mkono wa wote waliokuwa wakikunyanyasa. Niliwafukuza mbele yenu, na nimewapa nchi yao.
10Niliwaambia, “Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; Nimewaamuru msiabudu miungu ya Waamori, ambao mnaishi katika nchi yao. Lakini hamkuitii sauti yangu.”

Read Waamuzi 6Waamuzi 6
Compare Waamuzi 6:1-10Waamuzi 6:1-10