Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 25

Mambo ya Walawi 25:47-55

Help us?
Click on verse(s) to share them!
47Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,
48baada ya Mwisraeli mwenzako kuwa amenunuliwa. Anaweza kurejeshwa kwa maliopo. Iwapo anaweza kurejeshwa. Mtu fulani katika familia yake anaweza kumkomboa.
49Anaweza kuwa mjomba wake, au mjomba wa mwanawe, anayemkomboa yeye, au yeyote aliye ndugu yake wa karibu kutoka kwa ukoo wake. Au, iwapo ni mwenye mafanikio, anaweza kujikomboa mwenyewe.
50Ni lazima apatane na mtu aliyemnunua, itawapasa kuhesabu miaka tangu mwaka aliojiuza kwa mnunuzi wake mpaka mwaka wa Yubile. Ile thamani ya ukombozi wake ihesabiwe kulingana na kiwango cha mshahara anaolipwa mtumishi aliyeajiriwa, kwa idadi ya miaka ambayo angeweza kuendelea kufanya kazi kwa yule aliyemnunua.
51Endapo kutakuwa kungali na miaka mingi iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atalazimika kulipa fungu kubwa la fedha kwa ajili ya ukombozi ambao ni uwino wa idadi ya miaka hiyo.
52Iwapo kuna miaka michache tu iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atapatana na aliyemnunua ili kuipitia idadi ya miaka iliyobaki mpaka Yubile, naye atalazimika kulipia ukombozi wake kulingana na idadi ya miaka.
53Naye atatendewa kama mtu aliyeajiriwa mwaka kwa mwaka. Utahakikisha kwamba hatendewi kwa ukali.
54Iwapo hakukombolewa katika njia hizi, basi atatumika mpaka mwaka wa Yubile, yeye pamoja na watoto wake.
55Kwangu mimi watu wa Israeli ni watumishi. Wao ni watumishi wangu ambao Niliwatoa katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.

Read Mambo ya Walawi 25Mambo ya Walawi 25
Compare Mambo ya Walawi 25:47-55Mambo ya Walawi 25:47-55