Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 24

Mambo ya Walawi 24:13-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
13Kisha Yahweh akamwambia Musa,
14“Mchukue nje ya kambi huyo aliyemlaani Mungu. Wale wote waliomskia wataweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kusanyiko lote watamponda kwa mawe.
15Ni lazima uwaeleze watu wa Israeli na kusema, 'Yeyote anayemlaani Mungu wake imempasa kubeba hatia yake mwenyewe.
16Yeye anayelikufuru jina la Yahweh kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahweh, ni lazima auawe.
17Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auewa.
18Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.
19Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:
20Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.
21Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.
22Ni lazima mwe na sheria moja kwa wote, mgeni na Mwisraeli mwenyeji mzaliwa, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wanu.”
23Kwa hiyo Musa akazungumza na watu wa Israeli, nao watu wakamleta mwanaume huyo nje ya kambi, yule ambaye alikuwa amemlaani Yahweh. Wakampiga kwa mawe. Watu waisraeli wakaitekeleza amri ya Yahweh aliyoitoa kupitia Musa.

Read Mambo ya Walawi 24Mambo ya Walawi 24
Compare Mambo ya Walawi 24:13-23Mambo ya Walawi 24:13-23