17Zungumza na Aroni na umwambie, 'mtu yeyote wa ukoo wako katika vizazi vyako vyote mwenye kasoro mwilini mwake, asisogee kutoa chakula kwa Mungu wake.
18Mtu yeyote mwenye kasoro mwilini mwake asimkaribie Yahweh,
19mtu kama vile: kipofu au mtu asiyeweza kutembea, mtu aliyeharibiwa uso au kupungukiwa na viungo mwilini, mtu aliye na mguu au mkono wenye ulemavu,
20mtu mwenye kibiongo mgongoni mwake au aliye na kimo kidogo au wembamba usio wa kawaida, au mtu mwenye kasoro machoni mwake, au mwenye ugonjwa, kidonda, upele, au yule ambaye korodani zake zimeharibiwa.
21Hakutakuwa na mtu miongoni mwa ukoo wa Aroni kuhani mkuu mwenye kasoro mwilini atakayekaribia kutoa matoleo yatakayoteketezwa kwa moto kwa ajili ya Yahweh. Mtu kama huyo mwenye kasoro mwilini hatakaribia ili kutoa mkate wa Mungu wake.
22Anaweza kula chakula cha Mungu wake, ama iwe baadhi ya vile vilivyo vitakatifu sana au vile vitakatifu.
23Hata hivyo, hataingia ndani ya pazia wala kuisogelea madhabahu, kwa sababu ana kasoro mwilini mwake, ili kwamba asipanajisi mahali patakatifu pangu, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh anayewafanya watakatifu.”
24Kwa hiyo Musa akamwambia maneno haya Aroni, wanawe, na watu wote wa Israeli.