Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 10

Mambo ya Walawi 10:1-4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakachukua kila mtu kifukizo chake, akaweka moto ndani yake, na kisha uvumba. Kisha wakatoa moto usiokuabalika mbele za Yahweh, moto ambao hakuwaamru wao kuutoa.
2Kwa hiyo moto ukashuka chini mbele za Yahweh na kuwala, nao wakafa mbele za Yahweh.
3Kisha Musa akamwambia Aroni, Hivi ndiyo Yahweh alivyokuwa akizunguzia aliposema, 'Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.'” Naye Aroni hakusema neno lolote.
4Musa akamwita Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mjomba wa Aroni, naye akamwambia, “njoo huku na uwatowe ndugu zako nje ya kambi watoke mbele ya hema.”

Read Mambo ya Walawi 10Mambo ya Walawi 10
Compare Mambo ya Walawi 10:1-4Mambo ya Walawi 10:1-4