Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 5

Luka 5:7-38

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Hivyo wakawaashiria washirika wao kwenye mashua nyingine ili waja na kuwasaidia. Walikuja wakazijaza mashua zote, kiasi kwamba zikaanza kuzama.
8Lakini Simoni Petro, alipoona hivyo, alianguka magotini pa Yesu akisema, “Ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi Bwana.”
9Kwa sababu alishangazwa, na wote waliokuwa pamoja naye, kwa uvuvi wa samaki waliokuwa wameufanya.
10Hili liliwajumuisha Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo, ambao walikuwa washirika wa Simoni. Na Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea utavua watu.”
11Walipokwishazileta mashua zao nchi kavu, waliacha kila kitu na kumfuata yeye.
12Ilitokea kwamba alipokuwa katika mji mmojawapo, mtu aliyekuwa amejaa ukoma alikuwa huko. Wakati alipomuona Yesu, alianguka akiinamisha uso kwake mpaka chini na kumuomba, akisema, “Bwana, ikiwa unataka, waweza kunitakasa.”
13Kisha Yesu alinyoosha mkono wake na kumgusa, akisema, “Nataka. Takasika.” Na saa ileile ukoma ukamwacha.
14“Alimwagiza asimwambie mtu yeyote, lakini alimwambia, “Nenda zako, na ukajionyeshe kwa makuhani na utoe sadaka ya utakaso wako, sawasawa na kile Musa alichokiamuru, kwa ushuhuda kwao.”
15Lakini habari kumuhusu yeye zikaenea mbali zaidi, na umati mkubwa wa watu ukaja pamoja kumsikiliza akifundisha na kuponywa magonjwa yao.
16Lakini mara kwa mara alijitenga faraghani na kuomba.
17Ilitokea siku moja kati ya hizo siku alikuwa akifundisha, na walikuwapo Mafarisayo na waalimu wa sheria wamekaa hapo ambao walikuja wakitokea vijiji vingi tofauti katika mkoa wa Galilaya na Yudea, na pia kutokea katika mji wa Yerusalemu. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kuponya.
18watu kadhaa walikuja, wamembeba kwenye mkeka mtu aliyepooza, na wakatafuta njia ya kumwingiza ndani ili kumlaza chini mbele ya Yesu.
19Hawakupata njia ya kumwingiza ndani kwa sababu ya umati, hivyo walipanda juu ya paa la nyumba na kumshusha yule mtu chini kupitia kwenye vigae, juu mkeka wake katikati ya watu, mbele kabisa ya Yesu.
20Akiangalia imani yao, Yesu alisema, “Rafiki, dhambi zako umesamehewa.”
21Waandishi na Mafarisayo waliaanza kuhoji hilo, wakisema, “Huyu ni nani anayeongea makufuru? Ni nani anaweza kusamehe dhambi ila Mungu pekee yake?”
22Lakini Yesu, akitambua nini walichokuwa wakifikiri, aliwajibu na kuwaambia, “Kwa nini mnaulizana hili mioyoni mwenu?
23Kipi ni rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama utembee?'
24Lakini mjue ya kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi, Nakwambia wewe, 'Amka, chukua mkeka wako na uende nyumbani kwako.'”
25Wakati huo huo akaamka mbele yao na akachukua mkeka wake aliokuwa ameulalia. Kisha akariudi nyumbani kwake akimtukuza Mungu.
26Kila mmoja alishangazwa na wakamtukuza Mungu. Walijawa na hofu, wakisema, “Tumeona mambo yasiyo ya kawaida leo.”
27Baada ya mambo haya kutokea, Yesu alitoka huko na akamwona mtoza ushuru aliyeitwa Lawi amekaa eneo la kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate.”
28Hivyo Lawi akanyanyuka na kumfuata, akiacha kila kitu nyuma.
29Kisha Lawi akaandaa nyumbani kwake karamu kubwa kwa ajili ya Yesu. Walikuwapo watozaushuru wengi kule na watu wengi walioketi mezani wakila pamoja nao.
30Lakini Mafarisayo na waandishi wao walikuwa wakiwanung'unikia wanafunzi, wakisema, “Kwa nini mnakula na kunywa na watoza ushuru pamoja na watu wengine wenye dhambi?”
31Yesu akawajibu, “Watu walio katika afya njema hawahitaji tabibu, ni wale tu wanaoumwa ndiyo watakao mhitaji mmoja.
32Sikuja kuwaita watu wenye haki haki wapate kutubu, bali kuwaita wenye dhambi wapate kutubu.”
33Wakamwambia, “Wanafunzi wa Yohana mara nyingi hufunga na kuomba, na wanafunzi wa Mafarisayo nao hufanya vivyo hivyo. Lakini wanafunzi wako hula na kunywa.”
34Yesu akawaambia, “Inawezekana mtu yeyote akawafanya waliohudhuria harusi ya Bwana Arusi kufunga wakati Bwana Arusi bado yu pamoja nao?
35Lakini siku zitakuja wakati Bwana Arusi atakapoondolewa kwao, ndipo katika siku hizo watafunga.”
36Kisha Yesu aliongea pia kwao kwa mfano. “Hakuna anayechana kipande cha nguo kutoka kwenye vazi jipya na kukitumia kurekebisha vazi la zamani. Kama akifanya hivyo, ataichana nguo mpya, na kipande cha nguo kutoka vazi jipya kisengefaa kutumika na nguo ya vazi la zamani.
37pia, hakuna mtu ambaye huweka divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai mpya ingepasua kile chombo, na divai ingemwagika, na viriba vingeharibika.
38Lakini divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya.

Read Luka 5Luka 5
Compare Luka 5:7-38Luka 5:7-38