Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 17

Luka 17:12-30

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
13Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!”
14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.
15Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.
16Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.
17Hapo Yesu akasema, “Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?
18Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?”
19Halafu akamwambia huyo mtu, “Simama, uende zako; imani yako imekuponya.”
20Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu utakuja lini?” Naye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.
21Wala hakuna atakayeweza kusema, Uko hapa, au Uko pale. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu.”
22Halafu akawaambia wanafunzi wake, “Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
23Na watu watawaambieni: Tazameni yuko hapa; ninyi msitoke wala msiwafuate.
24Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
25Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.
26Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu.
27Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
28Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
29Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.
30Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.

Read Luka 17Luka 17
Compare Luka 17:12-30Luka 17:12-30