Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1Wafalme - 1Wafalme 22

1Wafalme 22:2-35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Ikawa katika mwaka wa tatu, Yehoshafati mfalme wa Israeli akashuka kwa mfalme wa Isreli.
3Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia watumishi wake, “Je, mnajua kuwa Ramothi Gileadi ni yetu, ila hatufanyi chochote kuitwaa kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Shamu?”
4Kwa hiyo akamwambia Yehoshafati, “Je, utakwenda na mimi katika vita huko Ramothi Gileadi?” Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, na farasi wangu ni kama farasi wako.”
5Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, “Tafadhali tafuta mwongozo kutoka neno la BWANA juu ya kile unachopaswa kufanya kwanza.”
6Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, walikuwa wanaume elfu nne, akawaambia, “Je, niende Ramothi Gileadi kupigana, au nisiende?” Nao wakamwambia, “Ivamie, kwa kuwa Bwana ataitoa katika mkono wa mfalme.”
7Lakini Yehoshafati akasema, “Je, hapa hayupo nabii mwingine wa BWANA ambaye tunaweza kupata ushauri?”
8Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Bado kuna mtu mmoja ambaye tunaweza kupata ushauri toka kwa BWANA ili kusaidia, Makaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu huwa hanitabirii mazuri yanayonihusu, ila hunitabiria matatizo tu.” Lakini Yehoshafat akasema, “mfalme na asiseme hivyo,”
9Kisha mfalme wa Israeli akmwita akida na akamwamuru, “Kamlete Makaya mwana wa Imla, sasa hivi.”
10Wakati huo Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi kila mmoja kwenye kiti cha enzi, wamevaa mavazi yao, katika eneo la wazi kwenye lango la kuingilia Samaria, na manabii walikuwa wakiwatabiria.
11Sedekia mwana wa Kenaana akajitengenezea pembe za chuma akasema, “BWANA asema hivi: 'Kwa hili utawasukuma Washami mpaka watakapoisha.'”
12Na manabii wengine wote wakasema hivyo, wakisema, “Ishambulie Ramothi Gileadi na ushinde, kwa kuwa BWANA ameiweka kwenye mkono wa mfalme.”
13Yule mjumbe aliyeenda kumwita Makaya akamwambia, akisema, “Tazama sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja wanatabiri mambo mema kwa mfalme. Tafadhali maneno yako yawe kama yao ukaseme mambo mazuri.”
14Makaya akajibu, “Kama BWANA aishivyo, kile BWANA atakachosema kwangu ndicho nitakachosema.'”
15Naye alipokuja kwa mfalme, mfalme akamwambia, “Makaya, je twende Ramothi Gileadi kupigana, au tusiende?” Makaya akamjibu, “Ivamie na ushinde. BWANA ataitoa kwenye mkono wa mfalme.”
16Kisha mfalme akamwambia. “Je, nikutake mara ngapi ili kuniapia ukweli kwa jna la BWANA?”
17Makaya akasema, “Ninaiona Israeli yote imesambaa kwenye milima, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji, na BWANA amesema, 'Hawa hawana mchungaji. Kila mtu na arudi nyumbani kwake kwa amani.'”
18Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Je sikukwambia kuwa huwa hanitabirii mambo mema yanayonihusu, ila majanga tu?”
19Kisha Makaya akasema, “Kwa hiyo sikiliza neno la BWANA: Nimemwona BWANA akiwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikuwa yamesimama karibu yake upande wake wa kulia na upande wake wa kushoto.
20BWANA akasema, 'Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili kwamba apande akafie Ramothi Gileadi? Na mtu mmoja akajibu kwa njia hii, na mwingine akajbu kwa njia ile.
21Ndipo pepo moja akajitokeza, akasimama mbele ya BWANA, akasema, 'Mimi nitamdanganya.' BWANA akmwuliza, 'Kwa jinsi gani?'
22Yule pepo akamjibu, 'Nitakwenda na kuwa roho idanganyayo katika vinywa vya manabii wake,' BWANA akamjibu, 'utaweza kumdanganya, na utafanikiwa. Nenda sasa ukafanye hivyo.'
23Tazama sasa, BWANA ameweka roho idangayo kwenye vinywa vya hawa manabii wako, na BWANA ametangaza janga kwako.”
24Kisha Sedekia mwana wa Kenaana, akaja, akamzabua Makaya shavuni, akasema, “Je, yule roho wa Bwana alitokaje kwangu ili asema na wewe?”
25Makaya akasema, “Tazama, “utatambua hilo katika siku hiyo, utakapokimbilia katika chumba cha ndani kujificha.”
26Mfalme wa Israeli akamwambia mtumishi wake, “Mkamate Makaya umpeleke kwa Amoni, liwali wa mji, na kwa mwanangu, Yoashi.
27Mwambie, 'mfalme anasema mweke huyo gerezani na awe anampa mkate kidogo na maji kidogo, mpaka nitakaporudi salama.'”
28Naye Makaya akasema, “Kama utarudi salama basi BWANA hajasema kupitia kinywa changu.” Na akaongeza, “Sikilizeni hili, ninyi watu.”
29Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati mfalme wa Yuda, wamepanda Ramothi Gileadi.
30Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe niende vitani, lakini wewe uvae vazi lako la kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na akaenda vitani.
31Naye mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru majemedari thelathini na mbili wa magari yake, akisema, “Msimwamgamize askari wa muhimu au ambaye si wa muhimu, badala yake mshambulieni mfalme wa Israeli tu.”
32Ikawa wakati majemedari wa magari walipomwona Yehoshafati wakasema, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Wakageuka ili kumshambulia, kwahiyo Yehoshafati akapiga kelele.
33Ikawa majemedari wa magari walipoona kuwa yeye hakuwa mfalme wa Israeli, wakamwacha.
34Lakini mtu mmoja akavuta upinde wake kwa kubahatisha na akampiga mfalme wa Israeli katikati ya mwunganiko wa mavazi yake ya chuma. Ahabu akamawambia dereva wa gari lake, “geuza unirudishe kutoka vitani, kwa kuwa nimeumizwa sana.”
35Vita ikawa mbaya sana siku hiyo na mfalme akalazwazwa garini mwake akiwakabili Washami. Akafa jioni hiyo. Damu ilimwagika kutoka kwenye jeraha lake ndani ya gari.

Read 1Wafalme 221Wafalme 22
Compare 1Wafalme 22:2-351Wafalme 22:2-35