Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 7

Yohana 7:3-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.
4Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”
5Hata ndugu zake pia hawakumwamini.
6Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.
7Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.
8Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.”
9Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
10Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
11Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?”
12Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.”
13Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
14Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
15Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, “Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.”

Read Yohana 7Yohana 7
Compare Yohana 7:3-15Yohana 7:3-15