Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 15

Yohana 15:5-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5“Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi yake. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo atazaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.
6Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue.
7Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa.
8Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu.
9Mimi nimewapenda ninyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu.
10Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

Read Yohana 15Yohana 15
Compare Yohana 15:5-10Yohana 15:5-10