Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mathayo

Mathayo 23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Baadaye aliongea na umati wa watu na wanafunzi wake. Akasema,
2“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa.
3Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya.
4Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba.
5Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao.
6Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi,
7na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa “Walimu” na watu.
8Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu.
9Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni.
10Wala msije kuitwa 'walimu,' kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo.
11Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.
12Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.
13Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo.
14(Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 “Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane”).
15Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ngambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo.
16Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao,, Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake.
17Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu?
18Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake.

19Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?
20Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.
21Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake.
22Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.
23Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka kwa bizali, mnaanaa na mchicha, lakini mnaacha mambo mazito ya sheria- haki, rehema, na imani. Lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya, na siyo kuacha mengine bila kuyatekeleza.
24Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!
25Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya vikombe na nje ya sahani, lakini ndani pamejaa dhuluma na kutokuwa na kiasi.
26Enyi Mafarisayo vipofu, safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili upande wa nje nao pia uwe safi.
27Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila kitu kilicho kichafu.
28Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu.
29Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.
30Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii.
31Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.
32Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.
33Enyi nyoka, wana wa vipiribao, kwa namna gani mtaikwepa hukumu ya jehanamu?
34Kwahiyo, tazama, nawatuma kwenu manabii, watu wenye hekima, na waandishi. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha. Na baadhi yao mtawachapa ndani ya masinagogi yenu na kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.
35Matokeo ni kwamba juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani, kuanzia damu ya Habili mwenye haki hadi kwa damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliye muua kati ya patakatifu na madhabahu.
36Kweli, nawaambieni, mambo haya yote yatakipata kizazi hiki.

37Yerusalemu, Yerusalemu, wewe unayewaua manabii na kuwapiga mawe wale ambao wanatumwa kwako! mara ngapi nimewakusanya watoto wako pamoja kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, lakini haukukubali!
38Tazama, nyumba yako imebaki ukiwa.
39Nami nakuambia, Kuanzia sasa na kuendelea hautaniona, hadi utakaposema, 'Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.”'