Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mathayo

Mathayo 17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe.
2Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.
3Tazama, pale walitokea Musa na Eliya wakiongea naye.
4Petro akajibu na kumwambia Yesu, “Bwana, ni vema kwetu sisi kuwepo mahali hapa. Kama ukitamani, nitajenga hapa vibanda vitatu - kimoja chako, na kimoja kwa ajili ya Musa, na kimoja kwa ajili ya Eliya.”
5Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni yeye.”
6Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana.
7Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, “Inukeni wala msiogope.”
8Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.
9Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akasema, “Msitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka katika wafu.”
10Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, “Ni kwanini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza?
11Yesu akawajibu na kusema, “Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote.
12Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao.”
13Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.
14Walipofika katika umati wa watu, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia,
15“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji.
16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.
17Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.”
18Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.

19Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, “Kwanini hatukuweza kumfukuza?”
20Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.
21(Zingatia: Maneno ya msitari wa 21 “Lakini, aina hii ya pepo haiwezekani kutoka, ila kwa maombi na Kufunga” hayaonekani katika nakala bora za kale).
22Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, “Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu.
23Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka.” Wanafunzi walihuzunika sana.
24Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, “Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?”
25Akasema, “Ndiyo” Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, “Unafikiria nini Simon? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawa kutoka kwa wageni?
26Na wakati Petro aliposema, “Kutoka kwa wageni” Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji.
27Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.