2na Yohana akiwa gereszani aliposikia akiwa juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,
3na wakamuuliza, “Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?”
4Yesu akajibu na kusema kwao “Nendeni mkamtaarifu Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.
5Watu wasioona wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, watu wasiosikia wanasikia tena, watu waliokufa wanafufuliwa kupata uhai, na watu wahitaji wanahubiriwa habari njema.