Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Marko - Marko 9

Marko 9:20-41

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Walimleta mtoto wake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni.
21Yesu alimwuliza baba yake, “Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?” Baba alisema, “Tangu utoto.
22Mara nyingine huanguka katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie.”
23Yesu alimwambia, “Kama uko tayari? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye.”
24Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, “Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.”
25Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, “wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru mwache, usiingie kwake tena.”
26Alilia kwa nguvu na kumhangaisha mtoto na roho alimtoka. Mtoto alionekana kama amekufa, Ndipo wengi walisema, “Amekufa,”
27Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mtoto alisimama.
28Wakati Yesu alipoingia ndani, wanafunzi wake walimwuliza faragha, “Kwa nini hatukuweza kumtoa?”
29Aliwaambia, “kwa namna hii hatoki isipokuwa kwa maombi.”
30Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo,
31kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, “Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.”
32Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza.
33Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”?
34Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
35Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.”
36Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema,
37“Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”
38Yohana alimwambia, “Mwalimu tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati.”
39Lakini Yesu alisema, “Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.
40Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.
41Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake.

Read Marko 9Marko 9
Compare Marko 9:20-41Marko 9:20-41