Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 5

Mambo ya Walawi 5:4-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Au kama yeyote akiapa bila kufikiri kwa midomo yake kufanya ubaya, au kufanya vyema kwa vyovyote vile mtu ameapa kwa haraka atakapotambua atakuwa na hatia kwa vitu hivyo.
5Mtu yeyote akiwa na hatia kwa vitu hivi, lazima akiri kwa yoyote dhambi aliyotenda.
6Ndipo atakapoleta sadaka yake ya hatia mbele za Bwana kwa dhambi aliyokwisha tenda. Ataleta kondoo jike au mbuzi kutoka katika kundi lake kuwa matoleo ya dhambi, kuhani atafanya upatanisho kuhusu dhambi yake.
7Kama hataweza kununua mwana kondoo ataleta kama sadaka ya hatia, hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana, mmoja kwa sadaka ya dhambi na mwingine ni sadaka ya kutekeketezwa.
8Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.
9Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.

Read Mambo ya Walawi 5Mambo ya Walawi 5
Compare Mambo ya Walawi 5:4-9Mambo ya Walawi 5:4-9