Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 17

Mambo ya Walawi 17:7-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.
8Ni lazima uwaambie, 'Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atoweye dhabihu
9na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'
10Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
11Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake. Nimeitoa damu yake kwenu kufanya upatanisho juu ya madhabahu kwa ajili ya uhai wenu, kwa sababu ni damu ndiyo ifanyayo upatanisho, kwa kuwa ni damu ipatanishayo kwa ajili ya uhai
12Kwa hiyo Niliwaambia Watu wa Israeli kwamba hayupo miongoni mwenu impasaye kula damu, wala yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu atakaye kula damu.
13Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mafumbi.
14Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyeote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.
15Mtu yeyote alaye mnyama aliyekufa au ambaye amelaruliwa na wanyama pori, ama yule mtu ni mwenyeji wa kuzaliwa au ni mgeni aishiye miongoni mwenu, ni lazima atazifua nguo zake na kujiosha katika maji, naye atakuwa najisi hata jioni. Kisha atakuwa safi.
16Lakini kama hazifui nguo zake au kuosha mwili wake, ni lazima aichukue hatia yake”.

Read Mambo ya Walawi 17Mambo ya Walawi 17
Compare Mambo ya Walawi 17:7-16Mambo ya Walawi 17:7-16