Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 15

Mambo ya Walawi 15:2-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2“Waambie watu wa Israeli, na sema kwao, 'Wakati mtu yeyote kisonono kimemwathiri mwili wake unatoa ugiligili, anakuwa najisi.
3Unajisi wake unatokana na athari ya kisonono. Iwe mwili wake unatoa ugiligili au umekoma, huo ni unajisi.”
4Kitanda chochote anachokilalia kitakuwa najisi, na kila kitu ambacho anakaa juu yake kitakuwa najisi.
5Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na awe amenajisika mpaka jioni.
6Yeyote anayekaa katika kitu chochote ambacho mtu ambaye ameathiriwa na kisonono alikaa, mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
7Na yeyote anayegusa mwili wa ambaye ameathirika na kisonono lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na awe najisi hadi jioni.
8Kama mtu ambaye anaona majimaji kama hayo kwa mtu fulani ambaye ametakasika, ndipo mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na atakuwa najisi hata jioni.
9Tandiko lolote ambalo ambaye anamajimaji ya kisonono atalikalia litakuwa najisi.
10Yeyote anayegusa kitu chochote kilichokuwa chini ya mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni, na yeyote anayebeba vitu hivyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji; atanajisika mpaka jioni.
11Ambaye anamajimaji kama hayo akimgusa kabla kwanza ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
12Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.
13Wakati mwenye kisonono anapotakaswa katika kisonono chake, ndipo lazima ahesabu kwaajili yake siku saba kwaajili ya kutakasika kwake; ndipo afue nguo na aoshe mwili wake kwenye maji yatiririkayo. Ndipo atakuwa safi.
14Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.
15Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe kwaajili ya kisonono chake.

Read Mambo ya Walawi 15Mambo ya Walawi 15
Compare Mambo ya Walawi 15:2-15Mambo ya Walawi 15:2-15