Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 24

Luka 24:36-52

Help us?
Click on verse(s) to share them!
36Wakati wakiongea mambo hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akawaambia, “Amani iwe kwenu.”
37Lakini waliogopa na kujawa na hofu, na wakafikiri kwamba waliona roho.
38Yesu akawaambia, Kwanini mnafadhaika? Kwanini maswali yanainuka mioyoni mwenu?
39Angalieni mikono yangu na miguu yangu, kwamba ni mimi mwenyewe. Niguseni na muone. Kwa maana roho haina nyama na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa navyo.”
40Alipokwisha kusema hivi, akawaonyesha mikono yake na miguu yake.
41Walipokuwa bado na furaha iliyochanganyikana na kutokuamini, na kustaajabu, Yesu akawaambia, “Je mna kitu chochote cha kula?”
42Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa.
43Yesu akakichukua, na kukila mbele yao.
44Akawaambia, “Nilipokuwa nanyi, niliwaambia kwamba yote yalioandikwa kwenye sheria ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimilike.”
45Kisha akafungua akili zao, kwamba waweze kuyaelewa maandiko.
46Akawaambia, “Kwamba imeandikwa, Kristo lazima ateseke, na kufufuka tena kutoka katika wafu siku ya tatu.
47Na toba na msamaha wa dhambi lazima ihubiriwe kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia kutokea Yerusalemu.
48Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
49Angalia, nawapelekea ahadi ya Baba yangu juu yenu. Lakini subirini hapa jijini, mpaka mtakapovishwa nguvu kutoka juu.
50Kisha Yesu akawaongoza nje mpaka walipokaribia Bethania. Akainua mikono yake juu, na akawabariki.
51Ikatokea kwamba, wakati alipokuwa akiwabariki, aliwaacha na akabebwa juu kuelekea mbinguni.
52Basi wakamwabudu, na kurudi Yerusalemu na furaha kuu.

Read Luka 24Luka 24
Compare Luka 24:36-52Luka 24:36-52