Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 21

Luka 21:25-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
25Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Na katika nchi kutakuwa na dhiki ya mataifa, katika kukata tamaa kutokana na mlio wa bahari na mawimbi.
26Kutakuwa na watu wakizimia kwa hofu na katika kutarajia mambo yatakoyo tokea juu ya dunia. Kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.
27Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija mawinguni katika nguvu na utukufu mkuu.
28Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu.”

Read Luka 21Luka 21
Compare Luka 21:25-28Luka 21:25-28