Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Wakorintho - 1 Wakorintho 7

1 Wakorintho 7:12-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.
13Kama mwanamke ana mme asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache.
14Kwa mme asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mmewe aaminiye. Vinginevyo watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.
15Lakini mwenzi asiyeamini akiondoka na aende. Kwa namna hiyo, kaka au dada hafungwi na viapo vyao. Mungu ametuita tuishi kwa amani.
16Unajuaje kama mwanamke, huenda utamwokoa mmeo? Au unajuaje kama mwanaume, huenda utamwokoa mkeo?
17Kila mmoja tu aishi maisha kama Bwana alivyowagawia, kila mmoja kama Mungu alivyowaita wao. Huu ni mwongozo wangu kwa makanisa yote.
18Yupo aliyekuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Hapaswi kutahiriwa.
19Kwa hili aidha ametahiriwa wala asiye tahiriwa hakuna matatizo. Chenye matatizo ni kutii amri za Mungu.
20Kila mmoja abaki katika wito alivyokuwa alipoitwa na Mungu kuamini.
21Ulikuwa mtumwa wakati Mungu alipokuita? Usijali kuhusu hiyo. Lakini kama unaweza kuwa huru, fanya hivyo.

Read 1 Wakorintho 71 Wakorintho 7
Compare 1 Wakorintho 7:12-211 Wakorintho 7:12-21