Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 9

Yohana 9:31-35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
31Tunajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini ikiwa mtu yeyote anamwabudu Mungu na hufanya mapenzi yake, Mungu humsikiliza.
32Tangu kuanza kwa Ulimwengu haijawahi kamwe kusikiwa kwamba yeyote ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingelifanya chochote.”
34Walijibu na kumwambia, “Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?” Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.
35Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, “Unamwamini Mwana wa Mtu?”

Read Yohana 9Yohana 9
Compare Yohana 9:31-35Yohana 9:31-35