Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 9

Yohana 9:2-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Basi, wanafunzi wakamwuliza, “Mwalimu! Ni nani aliyetenda dhambi: mtu huyu, ama wazazi wake, hata akazaliwa kipofu?”
3Yesu akajibu, “Jambo hili halikutukia kwa sababu ya dhambi zake yeye, wala dhambi za wazazi wake; ila alizaliwa kipofu ili nguvu ya Mungu ionekane ikifanya kazi ndani yake.
4Kukiwa bado mchana yatupasa kuendelea kufanya kazi za yule aliyenituma; maana usiku unakuja ambapo mtu hawezi kufanya kazi.
5Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu.”
6Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni,
7akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
8Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, “Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?”
9Baadhi yao wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi!”
10Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?”
11Naye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu. Basi, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona.”
12Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?” Naye akawajibu, “Mimi sijui!”
13Kisha wakampeleka huyo mtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo.
14Siku hiyo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho mtu huyo, ilikuwa siku ya Sabato.
15Basi, Mafarisayo wakamwuliza mtu huyo, “Umepataje kuona?” Naye akawaambia, “Alinipaka tope machoni, nami nikanawa na sasa naona.”

Read Yohana 9Yohana 9
Compare Yohana 9:2-15Yohana 9:2-15