Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 8

Yohana 8:50-59

Help us?
Click on verse(s) to share them!
50Mimi sijitafutii utukufu wangu mwenyewe; yuko mmoja mwenye kuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu.
51Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.”
52Basi, Wayahudi wakasema, “Sasa tunajua kweli kwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele!
53Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?”
54Yesu akawajibu, “Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu. Baba yangu ambaye ninyi mwasema ni Baba yenu, ndiye anayenitukuza.
55Ninyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika neno lake.
56Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi.”
57Basi, Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza miaka hamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?”
58Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko.”
59Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka Hekaluni.

Read Yohana 8Yohana 8
Compare Yohana 8:50-59Yohana 8:50-59