Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 7

Yohana 7:8-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujakamilika bado.鈥
9Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.
10Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.
11Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, 鈥淵uko wapi?鈥
12Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, 鈥淣i mtu mwema.鈥 Wengine walisema, 鈥淗apana, huwapotosha makutano.鈥
13Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
14Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
15Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, 鈥淜wa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.鈥
16Yesu akawajibu na kuwaambia, 鈥淢afundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
17Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
18Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
19Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?
20Makutano wakajibu, 鈥淯na pepo. Nani anataka kukuua?鈥
21Yesu akajibu na akawaambia, 鈥淣imetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.

Read Yohana 7Yohana 7
Compare Yohana 7:8-21Yohana 7:8-21