Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 4

Yohana 4:1-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane.
2(Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.)
3Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;
4na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.
5Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu.
6Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
7Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, “Nipatie maji ninywe.”
8(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)
9Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu.)
10Yesu akamjibu, “Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekwambia: Nipatie maji ninywe, ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai.”
11Huyo mama akasema, “Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai?

Read Yohana 4Yohana 4
Compare Yohana 4:1-11Yohana 4:1-11