Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wimbo wa Sulemani - Wimbo wa Sulemani 8

Wimbo wa Sulemani 8:6-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.
7Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe
8Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Nini tutamfanyia dada yetu siku hatakayo ahidiwa kuolewa?
9Kama ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
10Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
11Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao watalitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake.

Read Wimbo wa Sulemani 8Wimbo wa Sulemani 8
Compare Wimbo wa Sulemani 8:6-11Wimbo wa Sulemani 8:6-11