1Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliye nyonya ziwa la mama yangu. Ili kwamba kila ningekuona nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.
2Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, na utanifundisha. Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine
4Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza
5Ni nani huyu anaye kuja kutoka nyikani, amemuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe.