3Maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala.
4Shingo yako ni kama mnara wa pembe; macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni kwenye lango la Bathi Rabimu. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ambao watazama Damasko.
5Kichwa chako ni kama Karmeli; nywele kichwani mwako ni za zambarau nyeusi. Mfalme amestaajabishwa na vifundo vyake vya nywele.
6Jinsi gani ulivyo mzuri na wakupendeza, mpenzi, na mazuri yako.