6Hadi jioni ifike na vivuli viondoke, nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.
7Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
8Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya Amana, kutoka juu ya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, kutoka mashimo ya milima ya chuwi.
9Umeuiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeuiba moyo wangu, kwa mtazamo mmoja tu wako kwangu, kwa mkufu mmoja wa shingo yako.