1O, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; wewe ni mzuri. Macho yako ni ya hua nyuma kitamba chako cha uso. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likienda chini kutoka Mlima Gileadi.
2Meno yako ni kama kondoo walio nyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna ata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.