4Kisha nikaona kwamba kila tendo la kazi na kila kazi ya utashi ikawa wivu wa jirani ya mtu. Huu pia ni mvuke na kujaribu kuchunga upepo.
5Mpumbavu hukunja mikono yake na hafanyi kazi, hivyo chakula chake in mwili wake.
6Lakini afadhari konzi ya faida pamoja na kazi ya haraka kuliko konzi mbili pamoja na kazi ambayo hujaribu kuuchunga upepo.
7Kisha nikafikiri tena zaidi kuhusu ubatili, mvuke upoteao zaidi chini ya jua.
8Kuna aina ya mtu ambaye yuko peke yake. Hana mtu, hana mwana, wala ndugu. Hakuna mwisho wa kazi zake zote, na macho yake hayatosheki kwa kupata utajiri. Anashangaa, “Ninajishumbua na kuharibu furaha yangu kwa ajili ya nani?” Huu pia ni mvuke, hali mbaya.
9Watu wawili wanafanya vizuri zaidi ya mmoja; kwa pamoja wanaweza kupata malipo mazuri kwa ajili ya kazi yao.
10Kwa kuwa kama mmoja akianguka, mwingine anaweza kumwinua rafiki yake. Ingawa, huzuni humfuata yeye aliye peke yake anapoanguka kama hakuna mtu wa kumwinua.
11Na kama wawili wakilala pamoja, wanaweza kupata joto, lakini mtu mmoja anawezaje kupata joto akiwa mwenyewe?
12Mtu akiwa peke yake anaweza kushindwa nguvu, lakini wawili wanaweza kusimama katika shambulio, na kama ya nyuzi tatu haikatika upesi.
13Ni bora kuwa kijana masikini kuliko kuwa mfalme mzee na mpumbavu ambaye hajui jinsi ya kusikiliza maonyo.
14Hii ni kweli hata kama mtu mdogo anapokuwa mfalme kutoka gerezani, au hata kama alizaliwa masikini katika ufalme wake.
15Ingawa, niliona kila mmoja aliye kuwa hai na kuzunguka chini ya jua wakijitia chini kwa kijana mdogo aliyeinuka kama mfalme.