8Yeyote anayechimba shimo anaweza kutumbukia yake, na popote mtu anayevunja ukuja, nyoka anaweza kumuuma.
9Yeyote achongaye mwawe, anaweza kuumizwa nayo. Na mtu achongaye mbao, anaweza kujihatarisha kwa hiyo.
10Kama chuma bapa kisicho na makali, na mtu hainoi, kisha ni lazima atumie nguvu nyingi, lakini hekima hutoa faida kwa ufaulu.
11Kama nyoka akiuma kabla hajafurahi, hivyo hakuna faida kwa mfurahishaji.
12Maneno ya kinywa cha mtu mwenye hekima yana huruma. Lakini midomo ya mpumbavu humumeza mwenyewe.
13Kama maneno yanavyo anza kutiririka mdomoni mwa mpumbavu, ujinga hutoka, na mwisho mdomo wake hutiririka wazimu mbaya.
14Mpumbavu huongeza maneno, lakini hakuna ajuaye kinachokuja. Ni nani ajuaye baada yake?