Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Matendo - Matendo 1

Matendo 1:6-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Basi, mitume walipokutana pamoja na Yesu, walimwuliza, “Je Bwana, wakati huu ndipo utakaporudisha ule ufalme kwa Israeli?”
7Lakini Yesu akawaambia, “Nyakati na majira ya mambo hayo viko chini ya mamlaka ya Baba yangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.
8Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni ninyi, mtajazwa nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”
9Baada ya kusema hayo, wote wakiwa wanamtazama, alichukuliwa mbinguni; wingu likamficha wasimwone tena.

Read Matendo 1Matendo 1
Compare Matendo 1:6-9Matendo 1:6-9