Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Matendo - Matendo 19

Matendo 19:3-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Naye akasema, “Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?” Wakamjibu, “Ubatizo wa Yohane.”
4Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonyesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
5Baada ya kusikia hayo, walibatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
6Basi, Paulo akawawekea mikono, na Roho Mtakatifu akawashukia, wakaanza kusema lugha mbalimbali na kutangaza ujumbe wa Mungu.
7Wote jumla, walikuwa watu wapatao kumi na wawili.
8Kwa muda wa miezi mitatu Paulo alikuwa akienda katika sunagogi, akawa na majadiliano ya kuvutia sana juu ya Ufalme wa Mungu.
9Lakini wengine walikuwa wakaidi, wakakataa kuamini, wakaanza kuongea vibaya hadharani juu ya Njia ya Bwana. Hapo Paulo alivunja uhusiano nao, akawachukua pembeni wale wanafunzi wake, akawa anazungumza nao kila siku katika jumba la masomo la Turano.

Read Matendo 19Matendo 19
Compare Matendo 19:3-9Matendo 19:3-9