Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Matendo 19:2-5 in Swahili (individual language)

Help us?

Matendo 19:2-5 in Biblia Takatifu

2 Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Nao wakamjibu, “La! Hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatujasikia.”
3 Naye akasema, “Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?” Wakamjibu, “Ubatizo wa Yohane.”
4 Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonyesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.”
5 Baada ya kusikia hayo, walibatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
Matendo 19 in Biblia Takatifu

Matendo ya Mitume 19:2-5 in Biblia ya Kiswahili

2 Paulo akawaambia, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakamwambia, “Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu.”
3 Paul alisema, “Sasa ninyi mlibatizwaje?” Wakasema, “Katika ubatizo wa Yohana.
4 Basi Paulo akajibu, “Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu.”
5 Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.
Matendo ya Mitume 19 in Biblia ya Kiswahili