Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Marko - Marko 6

Marko 6:2-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, 鈥淛e, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
3Je, huyu si yule seremala mwana wa Maria, na ndugu yao kina Yakobo, Yose, Yuda na Simoni; Je, dada zake si wanaishi papa hapa kwetu?鈥 Basi, wakawa na mashaka naye.
4Yesu akawaambia, 鈥淣abii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake, kwa jamaa zake na nyumbani mwake.鈥
5Hakuweza kutenda miujiza hapo, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache, akawaponya.
6Alishangaa sana kwa sababu ya kutoamini kwao. Kisha Yesu alivitembelea vijiji vya pale karibu akiwafundisha watu.
7Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili, akaanza kuwatuma wawiliwawili. Aliwapa uwezo wa kuwatoa pepo wachafu,
8na kuwaamuru, 鈥淢sichukue chochote mnapokwenda isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni.
9Vaeni viatu lakini msivae kanzu mbili.鈥

Read Marko 6Marko 6
Compare Marko 6:2-9Marko 6:2-9