Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 8

Mambo ya Walawi 8:24-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
24Akawaleta wana wa Aroni, naye akaweka sehemu ya damu ya kondoo yule kwenye ncha ya sikio lao la kulia, kwenye dole gumba lao cha mkono wa kulia na kwenye kidole chao kikubwa cha mguu wa kulia. Kisha Musa akainyunyiza damu ya huyo kila upande wa madhabahu
25Naye akayatwaa yale mafuta, mafuta ya mkiani, mafuta liyolikuwa sehemu za ndani, na mafuta yafunikayo ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.
26Akachukua mkate mmoja kutoka kwenye kikapu cha mikate isiyo na hamira ambayoo ilikuwa mbele za Yahweh, akatwaa mkate moja usio na hamira, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na mkate mwemba wa kaki na akaiweka juu ya mafuta na juu ya paja la kulia la kondoo.
27Akaiweka yote mikoni mwa Aroni na katika mikono ya wanawe na kuitikisa mbele za Yahweh kuwa sadaka ya kutikiswa
28Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto.
29Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahweh. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru yeye.

Read Mambo ya Walawi 8Mambo ya Walawi 8
Compare Mambo ya Walawi 8:24-29Mambo ya Walawi 8:24-29