Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 18

Mambo ya Walawi 18:9-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Usilale na yeyote aliye mmoja miongoni mwa dada zako, ama ni binti ya baba yako au ni binti ya mama yako, ama aliyelelewa nyumbani mwenu au mbali nawe. Usilale na dada zako.
10Usilale na binti ya mwanao, au binti ya binti yako. Hiyo ingekuwa aibu yako mwenyewe.
11Usilale na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa kwa baba yako, yeye ni dada yako, na usilale naye.
12Usilale na dada ya baba yako. Yeye ni ndugu wa karibu kwa baba yako.
13Usilale na dada ya mama yako. Yeye ni ndugu wa mama yako.
14Usimfedheheshe ndug wa baba yako kwa kulala na mke wake. Usimkaribie kwa kusudi hilo; yeye ni shangazi yako.
15Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.
16Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.
17Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.
18Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.
19Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.
20Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jilani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.
21Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahweh.
22Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.
23Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama ye yote. Huo ungekuwa upotovu.
24Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.
25Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake
26Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagiza yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.
27Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.
28Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.
29Yeyote anayefanya mambo haya ya kuchukiza, watu wafanyao mambo hayo ya kuchukiza lazima watakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu wao.

Read Mambo ya Walawi 18Mambo ya Walawi 18
Compare Mambo ya Walawi 18:9-29Mambo ya Walawi 18:9-29