11Ambaye anamajimaji kama hayo akimgusa kabla kwanza ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
12Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.