Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 13

Mambo ya Walawi 13:3-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Naye kuhanai atachunguza ugonjwa huo kwenye ngozi ya mwili wake. Iwapo malaika zilizopo eneo lenye ugonjwa zimegeuka kuwa nyeupe, na iwapo ugonjwa umejitokeza juu ya ngozi, huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Baada cha kuhani kumchunguza, atamtangaza kuwa ni najisi.
4Iwapo lile doa ling'aalo katika ngozi yake ni jeupe, na kuonekana kwake halikwenda chini zaidi ya ngozi, na iwapo malaika za eneo lenye ugonjwa hazijabadilika kuwa nyeupe, naye kuhani atamtenga mgonjwa kwa siku saba.
5Katika siku ya saba, huyo kuhani itambidi kumchunguza tena ili kuona kama katika maamzi yake huo ugonjwa siyo mbaya, na kama haujaenea kwenye ngozi. Iwapo haujaenea, basi, kuhani atamtenga kwa siku saba zaidi.
6Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa ubepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.
7Lakini endapo ule upele utakuwa umishasambaa kwenye ngozi baada ya kuwa amejionyesha kwa kuhani kwa ajili kusafishwa kwake, itambidi kujionyesha tena kwa kuhani.
8Naye kuhani atamchunguza ilikuona kama huo upele umsambaa zaidi ndani ya ngozi. Na endapo utakuwa umesambaa, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
9Iwapo ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza umo kwa mtu fulani, naye mtu huyo yapasa aletwe kwa kuhan.
10Kuhani atamchunguza ili kuona kama kunauvimbe mweupe katika ngozi yake, endapo malaika zitakuwa zimebadilika kuwa nyeupe, au kumekuwa na nyama mbichi kwenye uvimbe.

Read Mambo ya Walawi 13Mambo ya Walawi 13
Compare Mambo ya Walawi 13:3-10Mambo ya Walawi 13:3-10