Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 20:19-24 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 20:19-24 in Biblia Takatifu

19 Walimu wa Sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
20 Basi, wakawa wanatafuta wakati wa kufaa. Wakawahonga watu fulani wajisingizie kuwa wema, wakawatuma wamnase Yesu kwa maswali, na hivyo waweze kumtia nguvuni na kumpeleka kwa wakuu wa serikali.
21 Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
22 Basi, twambie kama ni halali, au la, kulipa kodi kwa Kaisari!”
23 Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
24 “Nionyesheni sarafu. Je, sura na chapa ni vya nani?”
Luka 20 in Biblia Takatifu

Luka 20:19-24 in Biblia ya Kiswahili

19 Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.
20 Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
21 Nao wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
22 Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
23 Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
24 “Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, '“Ya Kaisari.”
Luka 20 in Biblia ya Kiswahili