Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 1:40-55 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 1:40-55 in Biblia Takatifu

40 Huko, aliingia katika nyumba ya Zakariya, akamsalimu Elisabeti.
41 Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifiu,
42 akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa.
43 Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?
44 Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha.
45 Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokwambia.”
46 Naye Maria akasema,
47 “Moyo wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
48 Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
49 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu, jina lake ni takatifu.
50 Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi.
51 Amefanya mambo makuu kwa mkono wake: amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
52 amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu.
53 Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
54 Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake.
55 Kama alivyowaahidia wazee wetu Abrahamu na wazawa wake hata milele.”
Luka 1 in Biblia Takatifu

Luka 1:40-55 in Biblia ya Kiswahili

40 Alikwenda nyumbani mwa Zekaria na akamsalimia Elizabeti.
41 Sasa, ilitokea kwamba Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka, na Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.
42 Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.
43 Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu ilipasa aje kwangu?
44 Kwa kuwa tazama, iliposikika masikoni mwangu sauti ya kusalimia kwako, mtoto tumboni mwangu akaruka kwa furaha.
45 Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.”
46 Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana,
47 na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
48 Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
49 Kwa maana yeye aliyemweza amefanya mambo makubwa kwangu, na jina lake ni takatifu.
50 Rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mheshimu yeye.
51 Ameonesha nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
52 Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
53 Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54 Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55 (kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”
Luka 1 in Biblia ya Kiswahili