Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 1

Luka 1:40-55

Help us?
Click on verse(s) to share them!
40Alikwenda nyumbani mwa Zekaria na akamsalimia Elizabeti.
41Sasa, ilitokea kwamba Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka, na Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.
42Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.
43Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu ilipasa aje kwangu?
44Kwa kuwa tazama, iliposikika masikoni mwangu sauti ya kusalimia kwako, mtoto tumboni mwangu akaruka kwa furaha.
45Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.”
46Mariamu akasema, nafsi yangu inamsifu Bwana,
47na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
48Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
49Kwa maana yeye aliyemweza amefanya mambo makubwa kwangu, na jina lake ni takatifu.
50Rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mheshimu yeye.
51Ameonesha nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
52Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
53Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55(kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”

Read Luka 1Luka 1
Compare Luka 1:40-55Luka 1:40-55