Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Luka - Luka 13

Luka 13:9-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza kuukata.”
10Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato.
11Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima.
12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umeponywa ugonjwa wako.”
13Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu.
14Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale, “Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato.”
15Hapo Bwana akamjibu, “Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato?
16Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo vyake siku ya Sabato?”
17Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda.

Read Luka 13Luka 13
Compare Luka 13:9-17Luka 13:9-17