Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 10

Luka 10:17-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”
18Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.
19Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.
20Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.”
21Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”
22“Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.”
23Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona.
24Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”
25Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?”
26Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”

Read Luka 10Luka 10
Compare Luka 10:17-26Luka 10:17-26