Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Luka 10:17-26 in Swahili (individual language)

Help us?

Luka 10:17-26 in Biblia Takatifu

17 Baadaye, wale sabini na wawili walirudi wamejaa furaha, wakisema, “Bwana, hata pepo wametutii tulipolitaja jina lako.”
18 Yeye akawaambia, “Nilimwona Shetani jinsi alivyokuwa anaporomoka kama umeme kutoka mbinguni.
19 Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaga nyoka na ng'e, na uwezo juu ya nguvu zote za yule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru.
20 Hata hivyo, msifurahi kwa sababu pepo wamewatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”
21 Saa ileile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akasema, “Nakushukuru ee Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na elimu mambo haya, ukawafumbulia wadogo. Naam, Baba, ndivyo ilivyokupendeza.”
22 Kisha akasema, “Baba yangu ameweka yote mikononi mwangu. Hakuna amjuaye Mwana ni nani ila Baba, wala amjuaye Baba ni nani ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anataka kumfunulia hayo.”
23 Halafu akawaelekea wafuasi wake akawaambia, “Heri wanaoona yale mnayoyaona ninyi!
24 Hakika, manabii na wafalme walitamani kuona yale mnayoyaona ninyi wasiyaone, na kusikia yale mnayoyasikia wasiyasikie.”
25 Baadaye mwalimu mmoja wa Sheria alisimama akamwuliza akitaka kumtega, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?”
26 Yesu akamwuliza, “Imeandikwa nini katika Sheria? Unaelewaje?”
Luka 10 in Biblia Takatifu

Luka 10:17-26 in Biblia ya Kiswahili

17 Wale sabini walirudi kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”
18 Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.
19 Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.
20 Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.”
21 Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”
22 “Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.”
23 Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona.
24 Ninawambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”
25 Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi izima wa milele?”
26 Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”
Luka 10 in Biblia ya Kiswahili