Text copied!
Bibles in Swahili (individual language)

Zaburi 73:1-18 in Swahili (individual language)

Help us?

Zaburi 73:1-18 in Biblia ya Kiswahili

1 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, kwa wale walio na moyo safi.
2 Lakini kwangu mimi, kidogo tu miguu yangu iteleze; miguu yangu karibu iteleze kutoka kwangu
3 kwa sababu niliwaonea wivu wenye kiburi nilipoona mafanikio ya waovu.
4 Kwa maana hawana maumivu hadi kufa kwao, lakini wana nguvu na wameshiba.
5 Wako huru dhidi ya mizigo ya watu wengine; nao hawateswi kama watu wengine.
6 Kiburi kinawapamba kama mkufu kwenye shingo zao; jeuri huwavika kama vazi.
7 Katika upofu wa jinsi hii dhambi huja; mawazo maovu hupita mioyoni mwao.
8 Wao hudhihaki na kuongea kwa namna ya uovu; kwa kiburi chao hutishia mateso.
9 Wameweka vinywa vyao dhidi ya mbingu, na ndimi zao hutanga tanga duniani.
10 Kwa hiyo watu wake huwageukia na maji yaliyojaa hukaushwa.
11 Nao husema, “Mungu anajuaje? Yako maarifa kwake yeye aliye juu?”
12 Fahamu: watu hawa ni waovu; mara zote hawajali, wakifanyika matajiri na matajiri.
13 Hakika nimeutunza moyo wangu bure na nimenawa mikono yangu pasipo kukosa.
14 Maana mchana kutwa nimeteswa na kuadhibiwa kila asubuhi.
15 Kama ningesema, “Ningesema mambo haya,” kumbe nigewasaliti kizazi hiki cha watoto wenu.
16 Ingawa nilijaribu kuyaelewa mambo haya, yalikuwa ni magumu sana kwangu.
17 Ndipo nilipoingia patakatifu pa Mungu na kuelewa hatma yao.
18 Hakika wewe huwaweka penye utelezi; huwaangusha mpaka palipoharibika.
Zaburi 73 in Biblia ya Kiswahili