8 Siku zake na ziwe chahe; mamlaka yake na yachukuliwe na mtu mwingine.
9 Watoto wake wawe yatima, na mke wake awe mjane.
10 Watoto wake wenye kutanga tanga na kuombaomba, wakiondoka katika nyumba zao zilizo haribika na kuomba chakula au pesa kwa wapita njia.
11 Mdai na achukue vitu vyake vyote amilikivyo; wageni wateke mapato ya kazi yake.
12 Asiwepo mtu yeyote wa kumfanyia wema; mtu yeyote asiwahurumie yatima wake.
13 Watoto wake waangamizwe; majina yao na yafutwe katika kizazi kijacho.
14 Uovu wa baba zake utajwe kwa Yahwe; na dhambi ya mama yake isisahaulike.
15 Hatia zao na ziwe mbele ya Yahwe siku zote; Yahwe na aiondoe kumbukumbu yao duniani.
16 Yahwe na afanye hivi kwa sababu mtu huyu kamwe hakusumbuka kuonesha uaminifu wa agano wowote, lakini badala yake aliwasumbua wanyonge, wahitaji, na kuwaua walio vunjika moyo.